Karibu

Karibu kwenye Tovuti ya CIL. Ligi ya Kutengwa inatoa huduma kwa Kaka na Dada za Christadelphian, na familia zao, ambao wametengwa na eklesia yao. Huduma hutolewa kwa ombi la eklesia yako, hata hivyo unaweza kufikia nyenzo zetu zote kwenye tovuti hii, iwe umejitenga au la.

Huduma zetu ni pamoja na:

  • Mawaidha ya mara kwa mara, Mafunzo ya Biblia na Mihadhara
  • Shule ya Jumapili na Shughuli za Vijana
  • Majarida ya Braille, vitabu na mawasiliano
  • Maktaba ya Rekodi za sauti na video
  • jukwaa la mikutano ya mtandaoni (CIL Meet)

Tafadhali wasiliana nasi ili kujua zaidi.

Ili kupata nyenzo zetu kwenye wavuti yetu, tafadhali jiandikishe na uingie . Unaweza kuona hakikisho hapa chini!

Sasisho za hivi karibuni

Katika Kumega Mkate

Jumapili, 30 Machi 2025

Hesabu 12-13; Methali 8-9; Luka 22 

La kushangaza, hatuna mara kwa mara nasaha zinazochunguza wahusika na matukio yaliyotokea kwenye Chakula Kile Cha Mwisho. Yesu alishiriki na wanafunzi wake chakula hicho, kabla ya kuuawa na kufufuka. 

Kwenye chakula hicho Yesu aliisimika kumbukumbu hii ya Kumega Mkate, tunayoitekeleza kila juma. Tutakiangalia kipindi cha kama masaa 36 kabla ya wakati huo. Maneno ya Yesu kwenye chumba kile cha juu, yanasemea umuhimu wa muda huo, katika huduma yake. Kwenye Luka 22:15 anasema: “Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu”. 

Upendo wa Baba

Jumapili, 23 Machi 2025
Tunao mbwa wawili nyumbani. Hivi karibuni wote walitoroka. Nilikuwa nimeusahau mlango wa mbele wazi, na dakika kadhaa zikapita kabla sijatambua hawako. Sikuwa najua ni wapi walipoelekea.

Unyeyekevu, Imani na Mbaraka

Jumapili, 16 Machi 2025

Walawi 24; Zaburi 131-134; Luka 7 

Kwenye Luka 7, Yesu yuko Galilaya akiwa na kazi nyingi. Inaelekea alikuwa sasa anaishi katika mji wa Kapernaumu; mji wa Petro na wengine. Kapernaumu ulikuwa kwenye pwani ya ziwa Galilaya, mahali ambapo baadhi ya wanafunzi walikuwa wakivua kujipatia riziki. 

Hapa tunamkuta kiongozi mmoja; akida, aliyekuwa mtu wa kimataifa, aliyekuwa akilipenda taifa la Kiyahudi. Hili halikuwa jambo la kawaida. Wazee wa Kiyahudi nao walikuwa wakimsemea vizuri; wanasema: “Analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi” (Luka 7:5). 

Sheria katika Picha

Jumapili, 09 Machi 2025

Walawi 16;  Zaburi 119:1-40;  2 Wakorintho 12-13 

Kwenye Kiebrania jina ‘Mambo ya Walawi’ tafsiri yake ni “Na aliita”. Kwa hiyo ni kitabu kinachowahusu wale wote ambao Mungu amewaita; kitabu cha ‘walioitwa’. 

Ndani yake tunaiona huruma ya Mungu kwa kuwa, yupo tayari kuishi na mwanadamu. Hili linaoneshwa na Hema la Kukutania, kama mahali pa kukutania pamoja naye. Katika hili ametoa pia njia inayokubalika kwake, ambamo mdhambi anaweza kumkaribia “YEYE asiyeweza kuitazama dhambi”; yaani Mungu.