Karibu

Karibu kwenye Tovuti ya CIL. Ligi ya Kutengwa inatoa huduma kwa Kaka na Dada za Christadelphian, na familia zao, ambao wametengwa na eklesia yao. Huduma hutolewa kwa ombi la eklesia yako, hata hivyo unaweza kufikia nyenzo zetu zote kwenye tovuti hii, iwe umejitenga au la.

Huduma zetu ni pamoja na:

  • Mawaidha ya mara kwa mara, Mafunzo ya Biblia na Mihadhara
  • Shule ya Jumapili na Shughuli za Vijana
  • Majarida ya Braille, vitabu na mawasiliano
  • Maktaba ya Rekodi za sauti na video
  • jukwaa la mikutano ya mtandaoni (CIL Meet)

Tafadhali wasiliana nasi ili kujua zaidi.

Ili kupata nyenzo zetu kwenye wavuti yetu, tafadhali jiandikishe na uingie . Unaweza kuona hakikisho hapa chini!

Sasisho za hivi karibuni

Neno moja

Jumapili, 12 Januari 2025

Mwanzo 22-23;  Zaburi 26-28; Mathayo 14 

Kuna wepesi unaosisimua kwa namna Daudi anavyochukulia mambo kwenye Zaburi ya 27:4. Anasema:         “Neno moja nimelitaka kwa BWANA, nalo ndilo nitakalolitafuta; nikae nyumbani mwa BWANA siku zote za maisha yangu, niutazamie uzuri wa BWANA, na kutafakari hekaluni mwake”. 

Ni mawazo mengi yanayopita vichwani mwetu kila siku. Lakini ukweli ni kwamba, tunaweza tu kufikiria jambo moja kwa wakati mmoja. Sasa, tunawezaje kuyaweka sawa mahitaji ya mambo tunayoyafikiria na mambo tunayoyaamini sana? 

Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki

Jumapili, 05 Januari 2025

Mwanzo 9 -10;  Zaburi 11 – 13;  Mathayo 7 

Tunavyouanza mwaka mpya na kuanza tena kuzisoma sura za mwanzo katika kitabu cha Mwanzo, haraka tunakumbuka kuwa sisi ni wadhaifu sana. 

Tunapungukiwa na mengi. Hili linatufanya tushindwe kumpa Baba yetu wa Mbinguni utukufu, jambo lililokuwa la msingi kabisa katika kumuumba mwanadamu juu ya dunia. Kwenye Mwanzo 3 tunasoma jinsi mwanadamu alivyoanguka. 

Sefania - Masomo kwa Siku za Mwisho

Jumapili, 29 Desemba 2024

Ayubu 39;  Malaki; Ufunuo 17-18 

Kwa ajili ya nasaha, ningependa nichukulie mawazo yetu kutoka kwa nabii Sefania. Ni kitabu kidogo, lakini chenye unabii mzito. Tunaangalia kidogo kwenye sura ya kwanza, tuweze kupata mafundisho ya jumla yanayotufaa katika siku zetu hizi. 

Sefania alitoa unabii wake katika siku za Yosia, mfalme wa Yuda, wakati ufalme huo ulipokuwa ukikaribia kuvunjwa. Ulikuwa ni ujumbe wa siku za mwisho kwa kizazi hicho. Tutaona unafanana na siku zingine ‘za mwisho’ kama zilivyo katika Biblia. Ni siku zetu hizi. 

Laodikia

Jumapili, 22 Desemba 2024

Ayubu 29-30;  Zekaria 6-7;  Ufunuo 3-4  

Mojawapo ya changamoto kubwa tunayokuwa nayo katika ufuasi wetu wa kila siku, ni kukumbuka kilicho muhimu katika maisha yetu. Ni rahisi sana kutekwa na kuvutwa, kufuata mambo mengine yaliyopo na yanayojileta kwetu. Matokeo yake, maisha yetu ya kiroho yanaumia. 

Mojawapo ya mambo aliyosemea sana Yesu mwishoni mwa huduma yake ni hili. Alikazia haja ya sisi kuweka mbele yetu ukweli wa Ufalme unaokuja; ambao kwa hakika hauko mbali sasa. Anasema, kwa mfano: 

Maisha na kifo cha Bwana Yesu Kristo

Jumapili, 15 Desemba 2024

Ayubu 18-19;  Sefania 1; 2 Petro 3 

Matukio yaliyozunguka kuzaliwa kwa Yesu yametajwa katika sehemu mbili tu katika Biblia; katika Injili ya Mathayo na ya Luka. La msingi katika kuzaliwa kwake ilikuwa kwamba, alikuwa ni Mwana wa Mungu. Tunahitaji kuelewa kuwa, huu ulikuwa muujiza wa ajabu sana, na hakuna namna tunavyoweza kuuelezea vile hasa ulivyotokea. 

Kwa hiyo tunahitaji kukubali tu kwa kuamini kuwa Yesu alikuwa Mwana wa Mungu. Matukio yote yalipoanzia ni katika Mariamu kufunikwa na nguvu ya Mungu; Roho yake Takatifu. Hili ni wazi linaelezea kuwa Yesu hakuzaliwa kwa mwanamume na mwanamke kuja pamoja, kama inavyotokea watoto wanapozaliwa. 

“Kupendelea watu”

Jumapili, 08 Desemba 2024
Respecters of Persons

Ayubu 10; Mika 6; Yakobo 2

“Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu. Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri, kisha akaingia na maskini mwenye mavazi mabovu, nanyi mkamstahi yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri, na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale au keti miguuni pangu, Je! hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?” (Yakobo 2:1-4).