Karibu

Karibu kwenye Tovuti ya CIL. Ligi ya Kutengwa inatoa huduma kwa Kaka na Dada za Christadelphian, na familia zao, ambao wametengwa na eklesia yao. Huduma hutolewa kwa ombi la eklesia yako, hata hivyo unaweza kufikia nyenzo zetu zote kwenye tovuti hii, iwe umejitenga au la.

Huduma zetu ni pamoja na:

  • Mawaidha ya mara kwa mara, Mafunzo ya Biblia na Mihadhara
  • Shule ya Jumapili na Shughuli za Vijana
  • Majarida ya Braille, vitabu na mawasiliano
  • Maktaba ya Rekodi za sauti na video
  • jukwaa la mikutano ya mtandaoni (CIL Meet)

Tafadhali wasiliana nasi ili kujua zaidi.

Ili kupata nyenzo zetu kwenye wavuti yetu, tafadhali jiandikishe na uingie . Unaweza kuona hakikisho hapa chini!

Sasisho za hivi karibuni

Unyeyekevu, Imani na Mbaraka

Jumapili, 16 Machi 2025

Walawi 24; Zaburi 131-134; Luka 7 

Kwenye Luka 7, Yesu yuko Galilaya akiwa na kazi nyingi. Inaelekea alikuwa sasa anaishi katika mji wa Kapernaumu; mji wa Petro na wengine. Kapernaumu ulikuwa kwenye pwani ya ziwa Galilaya, mahali ambapo baadhi ya wanafunzi walikuwa wakivua kujipatia riziki. 

Hapa tunamkuta kiongozi mmoja; akida, aliyekuwa mtu wa kimataifa, aliyekuwa akilipenda taifa la Kiyahudi. Hili halikuwa jambo la kawaida. Wazee wa Kiyahudi nao walikuwa wakimsemea vizuri; wanasema: “Analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi” (Luka 7:5). 

Sheria katika Picha

Jumapili, 09 Machi 2025

Walawi 16;  Zaburi 119:1-40;  2 Wakorintho 12-13 

Kwenye Kiebrania jina ‘Mambo ya Walawi’ tafsiri yake ni “Na aliita”. Kwa hiyo ni kitabu kinachowahusu wale wote ambao Mungu amewaita; kitabu cha ‘walioitwa’. 

Ndani yake tunaiona huruma ya Mungu kwa kuwa, yupo tayari kuishi na mwanadamu. Hili linaoneshwa na Hema la Kukutania, kama mahali pa kukutania pamoja naye. Katika hili ametoa pia njia inayokubalika kwake, ambamo mdhambi anaweza kumkaribia “YEYE asiyeweza kuitazama dhambi”; yaani Mungu. 

Ufufuo wa Wafu

Jumapili, 02 Machi 2025

Masomo: Walawi 7; Zaburi  106; 1 Wakorintho 15 

Katika Waraka wa kwanza kwa Wakorintho, Sura ya 15, mtume Paulo anaandika akiongozwa na Roho, juu ya Ufufuo. Ni mada inayosisimua sana, kwa kuwa tunaishi kwenye dunia ya dhambi, magonjwa na kifo. 

Makaburi yetu ni ushuhuda wa uharibifu na uozo, ambao ni hatma ya maisha yetu mafupi. Lakini, tumaini la ufufuo, kama tutakavyoona, ni kitu cha uhakika. Ni kitu cha msingi kwenye imani yetu kuhusiana na kuja kwa Ufalme, na tunapata faraja na tumaini hasa miaka yetu inapoporomokea uzeeni. 

“Heri Leo Msikie Sauti Yake”

Jumapili, 23 Februari 2025

Masomo: Kutoka 36; Zaburi 94-95;  1 Wakorintho 6 

Imekuwa hivi hivi wakati wote; wenye kiburi na waovu wamewashinda wenye haki. Wanawafanya walie “mpaka lini?” Wanapolia wanajiuliza hili litapita lini! 

Kuna kuchoshwa na mateso watu-wa-imani, wanavyoona waovu wakiwakalia wanyonge kwa nguvu na mambo yao kuwanyokea. Lakini imekuwa hivi tangu zamani, balaa lilipoingia kwenye Bustani ya Edeni, wakati nyoka alipomlaghai Hawa na Kaini kumuua Habili. 

Kumjengea Mungu Madhabahu

Jumapili, 16 Februari 2025
Kutoka 27 inaanza na maelekezo ya ujenzi wa madhabahu ya dhabihu za kuchomwa. Inasemea vitu vilivyohitajika na vilivyounganishwa. Nasi tumeunganishwa katika Kristo.

Vita ya Amaleki na BWANA

Jumapili, 09 Februari 2025

Masomo: Kutoka 17-18; Zaburi 72; Marko 5 

Kutoka kwa Israeli Misri na safari yao ya nyikani, yana mafundisho mengi kwetu katika ufuasi wetu. Siku waliyogongana na kabila la Waamaleki imeelezewa kwenye somo letu la Kutoka 17, linalohitaji kupitiwa kwa umakini. Andiko linasema ilikuwa ni siku ya kukumbukwa daima. Lakini kwa nini?